Ticker

6/recent/ticker-posts

BREAKING NEWS:SERIKALI YAPIGA MARUFUKU SIMBA NA YANGA KUTUMIA UWANJA WA TAIFA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.2,2016 SAA 12:30 MCHANA

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye ametangaza kupiga marufuku klabu za Simba na Yanga
kutumia uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana.

Waziri Nape ametangaza kuchukuwa uamuzi huo mapema hii leo Hasubui mara baada ya kutembelea uwanja wa Taifa na kubaini uharibifu mkubwa unaosemekana kufanywa na  mashabiki wa Simba waliong'oa Viti katika  uwanja wa Taifa wakati wa mechi ya watani hao wa  jadi mchezo uliopigwa hapo jana na kumalizika kwa sare ya 1-1.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye akikagua uhalibifu uliofanya hapo jana na mashabiki wanaosemekana kuwa ni wa Simba
"Ukitaka kukomesha uhuni lazima uchukuwe hatua kubwa sana,tunataka tuuwe huu ujinga unauondelea kufanyika,na hili litakuwa ni fundisho,siyo hapa tu,hata maeneo mengine yanye viti kama hivi"alisema Nape Nauye.

Takribani Viti 1,781 vilivyokuwa katika jukwaa la klabu ya Simba Vimeng'olewa siku ya jana katika mchezo huo 

Nape pia amesema uhalibufu  uliofanyika hapo jana Klabu husika zitalipa na watakamata mgao wao mpaka watapohakikisha kuwa wamelipa gharama zote. 

Simba na Yanga hawatatumia uwanja wa Taifa kwa mechi na Timu yeyote ile,lakini wanaweza kutumia viwanja vingine kama Uhuru N.K

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)


Post a Comment

0 Comments