Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.11,2016 SAA 02:15 USIKU
Waziri wa habari Sanaa utamaduni na michezo Nape Nnauye hi
leo amezindua mfumo matumizi ya Tiketi za kielectroniki katika
uwanja wa taifa
jijii Dar es salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo Nape Nnauye amesema kuwa
Mfumo huo kuwekwa katika kiwanja cha Taifa ni muendelezo wa serikali kuwekeza
katika michezo na kuhakikisha sekta ya
michezo inasonga mbele.
Nape pia amewataka watanzania kujivunia mfumo huo kwani ni
moja ya mifumo bora iliyowekwa katika viwanja kwa nchi za ukanda wa kusini mwa
jangwa la sahara.
Nape pia amewataka watanzania kutambua kuwa kuwekwa kwa
mfumo huo ni moja ya sehemu ya gharama za uwanja huo.
kampuni ya Selcom ni
kampuni ya kitanzania ndiyo iliyopewa dhamana ya kufunga mitambo hiyo ya tiketi
za kielecteronini.
Kwa upande wa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF ambao
ni wadau wakubwa wa uwanja huo,kwa kupitia rais wake Jamali Malinzi,ameiomba
serikali kutumia mfumo huo kwa kuangalia Zaidi maslai ya vilabu.
Sambamba na hilo Jamali malinzi ameelezea changamoto mbali
mbali walizokutananazo kwa mara ya kwanza walipoutumia mfumfumo huo na kutoa wito kwa Serikali kuzifanyia kazi.
Kwa upande wa vilabu vya ligi kuu Tanzania Bara,Jamii na Michezo imezungumza na Katibu mkuu wa klabu ya Simba Patrick kahemelea ambaye wao wameupokea kwa moyo mkunjufu mfumo huo mfumo huo.
Kwa upande wa mchezo wa Netball ambapo viwanja vyao navyo
vipo katika uwanja wa huo wa Taifa ,Jamii na michezo imezungumza na mwenyekiti wa chama cha
mchezo huo Zainabu Mbilo,ambaye amesema kwa sasa wako katika mchakato wa
kuhakikisha mchezo huo unapata udhamini ili wanapocheza katika uwanja
huo,mchezo huo uwe pia na viingilio na kupata fedha za kuendeleza mchezo huo.
ANGALIA PICHA
0 Comments