Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:SIMBA SC YAREJEA KILELE KWA KISHINDO,AJIBU,MAVUGO WANG'ARA

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.11,2016 SAA 02:36 USIKU

Klabu ya Simba imeendelea kujiimalisha katika Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara baada ya kuchomoka na ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya leo  jumapili katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba hii leo yamefungwa na Ibrahim Hajib  dakika ya 52 kwa kichwa akimalizia kona nzuri iliyochongwa na beki Mohammed Hussein 'Tshabalala', pamoja na Laudit Mavugo dakika ya 66 akiwa ndani ya boksi baada ya pasi ya kiungo Mwinyi Kazimoto  Mabao yote yamefungwa kipindi cha pili.
Simba SC imefikisha alama 10 baada ya kucheza mechi nne, wakishinda tatu na sare moja. 

African Lyon ya Dar es Salaam  kesho Septemba 12, 2016 itaikaribisha Mbao FC kwenye mchezo Mchezo huo Na. 28 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaofanyika Uwanja wa Uhuru jijini. 
Mara baada ya mechi hiyo, raundi ya tano itafanyika mwishoni mwa wiki ijayo kadiri ya ratiba.

ANGALIA PICHA


KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments