Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.12,2016 SAA 01:35 USIKU
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya Azam FC na
Simba ya Dar es Salaam, utafanyika Jumatano
Septemba 21, 2016 badala ya
Septemba 17, mwaka huu.
Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam, umesogezwa mbele kuipisha timu ya taifa ya
Congo-Brazzaville ambao watacheza na Serengeti Boys,ili ipate nafasi ya kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa
Taifa, ikiwa ni kutekeleza matakwa ya kanuni za mchezo wa mpira wa miguu
za kimataifa kwamba mwenyeji lazima aachie uwanja siku moja au saa 24
kabla ya mchezo wa ushindani.
0 Comments