Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.12,2016 SAA 01:54 USIKU
African Lyon ya Dar es Salaam hii leo Septemba 12, 2016 imeitandika Mbao
FC mabao 3 kwa 1 kwenye Mchezo huo
Na. 28 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
uliofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Mbao FC ndiyo walikuwa wakwanza kupata bao dakika 28 kupitia kwa Frank Msiba
Lakini sekunde chache kabla ya kwenda mapumziko Hood Mayanja akaisawazishia African Lyon.
Kipindi cha pili dakika 58 African Lyon wakapata penalti iliyopigwa na mfungaji wa bao lao kwanza Hood Mayanja.na bap la tatu la African Lyon likafungwa na Tito Okello dakika 68.
0 Comments