Mario Balotelli ameonyesha mtazamo sahihi na njaa ya kufanikiwa kama mchezaji wa Liverpool , kwa mujibu wa meneja msaidizi wa
klabu hiyo Colin Pascoe.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia ana bao moja tu katika mechi 11 tangu asajiliwe kwa £ 16m kwa klabu hiyo ya Anfield kutoka AC Milan,huku Waandishi wengi wa Vitabu wakamdharau Balotelli kwa uchezaji wake wa hivi karibuni.
Akizungumza kabla ya Liverpool kucheza mechi ya nne ya Capital One Cup dhidi ya Swansea katika uwanja wa Anfield siku ya Jumanne hii leo, Pascoe alisisitiza kuwa wafanyakazi wa klabu hiyo wanamsaidia Balotelli kurudi katika fomu yake ya Ubora.
"anafanya kazi kwa bidii,ana kipaji kikibwa na kila siku katika mazoezi unaweza kuona jinsi anavyotaka kufanya juhudi zaidi," alisema Pascoe.
"Kila kitu kitakuwa vizuri kwa Mario kwa sababu unajua njaa yake ni pale yeye anapotaka kushinda".
"Baada ya kila kipindi cha mazoezi anataka kupiga mashuti, pasi- anataka kufanya kila kitu, kwa kazi ya mchezo wake Sisi kama makocha tunamsaidia kwa njia hiyo."
Lakini Pascoe alikataa kuzungumzia kama mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 atakuwa katika kikosi cha mapigano dhidi ya Swansea ya kocha Garry Monk siku ya Jumanne usiku.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments