Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amesema kwamba ushangiliaji wa goli wa Robin van Persie dhidi
ya Chelsea siku ya Jumapili,ulikuwa ni wa "kijinga "
Mshambuliaji huyo wa Uholanzi aliiokoa United na kipigo katika dimba la Old Trafford, kufutia kongozwa kwa bao moja na Chelsea lililofungwa na Didier Drogba, huku wakibakisha dakika kadhaa kumaliza mchezo katika muda wa majeruhi.
Van Persie alivua haraka shati lake kwa furaha baada ya kufunga bao la kusawazisha, na mwamuzi Phil Dowd akamuonesha kadi ya njano kama tahadhari ,ambayo ili mchanganya bosi wake.
"Ilikuwa ni kitendo cha kijinga baada ya kufunga," Van Gaal aliviambia vyombo vya habari.
"Mimi naona alishtuka lakini baada ya kadi, haikuwa hustaharabu."
Bao la van Persie lilikuwa ni la tatu kwake kwa klabu yake msimu huu,katika mchezo wake wa nane na kuwapatia mashteni wekundu pointi 13, alama tatu nyuma ya West Ham walioko nafasi ya nne.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments