Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.10,2016 SAA 05:16 USIKU
Klabu ya YANGA imechomoka na ushindi wa mabao 3 - 0 Dhidi ya Majimaji ya Songea katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara uliopigwa leo katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Tanzania Bara uliopigwa leo katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Amissi Tambwe ambaye ni Mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, alifunga mabao mawili dakika ya kipindi cha pili baada ya kiungo Deus David Kaseke kutangulia kufunga kipindi cha kwanza.
Simon Msuva alipiga penalti mbili ambazo alifunga, lakini refa akamuamuru kurudia baada ya kusema kuwa wachezaji wenzake walisogea kabla ya kupiga.
Refa alimwambia Msuva apige penalti kwa mara yatatu, shuti ambalo liligonga mwamba na kurudi uwanjani papo hapo kukatokea purukushani na mpira kumkuta Kaseka ambaye aliyefunga bao.
Yanga imefikisha pointi saba, baada ya kucheza mecni tatu, ikishinda mbili na kutoka sare mechi moja sawa na mahasimu wao, Simba SC.
Matokeo mengine Mbeya City 1-2 Azam
ANGALIA PICHA
0 Comments