Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:NAPE ATIMBA TFF NA KUPATA UFAFANUZI WA DENI LA MKWASA NA WAFANYAKAZI

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.10,2016 SAA 08:16 MCHANA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (MB) hii leo Jumamosi Septemba 10, ametembelea za
Ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.

 Waziri Nape alizungumza na Mwenyeji wake Rais wa Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji pamoja na Sekretarieti kisha kuzungumza na Waandishi wa Habari ambao TFF iliwaalika katika ziara hiyo.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari Nape Nnauye amesema Amefurahi kupata muda wa kutembelea TFF,kwani tangu achaguliwe kuwa waziri,ameona aje kuona kazi zao na kushauriana mambo macheche ,Nape amesema kama serikali wanaipongeza tff kwa mipango iliyopangwa,na serikali inaamini kama wakiwekeza kutokea chini wanaweza kufaidika.
"watu wanadhani tff inafedha nyingi, lakini ukiona maneno mengi unatafuta njia ya kushughulika".alisema Nape

Nape anasema Wizara yake ilimuagiza mkaguzi mkuu wa serikali kufanya ukaguzi mkubwa wa kuangalia rasilimali fedha na watu kwa Tff,na kwa rasimilimali watu inasemekana kuna watumishi wanadai mishahara,Jambo ambalo Rais wa Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi alikiri kwa kusema kuna baadhi ya watumishi kweli hawajalipwa mishahara yao ya mwezi mmoja huku pia akigusia Swala la kocha mkuu Chalse Boniface Mkwasa akisema kulitokea matatizo ya kimfumo katika ulipwaji wake lakini muda si mrefu mambo yatakaa sawa.

"Kutokana na mabadiliko ya kimfumo,kuna baadhi ya malipo ya wafanyakazi ya hayajalipwa"alisema Jamal Emil Malinzi

Eneo lingine alilolizungumzia Nape ni Kuhusu mchakato wa uchaguzi,ambapo pia amempongeza raisi kwa kuchaguliwa na chama cha soka Mkoani kagera,huku akisema Tff iliwaahidi watasimamia uchaguzi,basi wahakikishe kamati zinakuwa huru kwa kusimamimia uchaguzi kwa haki na huru.
Eneo lingine alilozungumzia malinzi ni mchakato wa mabadiliko ya mifumo ya uwendeshaji wa Virabu,Nape amesema Kama serikali inaunga mkono kwa mabadiliko chanya,lakini michakato hiyo iwe ya uwazi kwa kila linalofanyika  na sharia na taratibu zifuatwe,lakini  pia ametoa ushauri kwa vilabu kujua thamani ya vilabu vyao kabla ya kuuziana au kukodishanya,lakini pia amesema ni vizuri kujua Hadhi ya vilabu hivyo .
“Tff isisubiri mpaka Jipu Liive,inapaswa kuchukuwa hatua mapema,mkiona jambo haliendi sawa elekezeni ili mambo yanyooke,kama  serikali hatuoni shida kwenda katika mfumo wa mabadiliko”alisisitiza Nape 


Swala la migogoro ya mara kwa mara ya klabu ya Yanga na Tff.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (MB) amesema kuwa ,mahusiano kati Ya Yanga na Tff,kama serikali inatoa Rai kuacha marumbano,na kusisitiza kuwa inapaswa kuendesha michezo kwa kutumia misingi,na tff isisubiri mpaka jambo liaribike, na kuwaambia kwamba Tff wakiona jambo haliendi sawa basi watoe adhabu.


KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments