Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.21,2016 SAA 11:17 JIONI
Mechi mbili za raundi ya sita za Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na
Majimaji, na African Lyon na Kagera Sugar sasa
zitachezwa kwenye Uwanja
wa Taifa badala ya Uwanja wa Uhuru.
Mabadiliko hayo yametokana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) kusitisha kwa muda kuutumia Uwanja wa Uhuru katika kipindi hiki
ambacho limeanza kufanyia marekebisho sehemu ya uwanja huo ambayo ni ya
nyasi bandia (artificial turf).
Hivyo, mechi ya Simba na Majimaji itafanyika Jumamosi, Septemba 24
wakati ile ya African Lyon na Kagera Sugar itachezwa Jumatatu, Septemba
26. Jumapili, Septemba 25 Uwanja Taifa utatumiwa kwa mechi ya timu za
Wabunge za Simba na Yanga ili kuchangia waathirika wa janga la tetemeko
lililotokea mkoani Kagera.
Mechi nyingine za Ligi Kuu ya Vodacom zitakazochezwa Jumamosi,
Septemba 24 ni kati ya JKT Ruvu na Mbeya City (Mabatini), Ndanda na Azam
(Nangwanda Sijaona), Tanzania Prisons na Mwadui (Sokoine), Mtibwa Sugar
na Mbao (Manungu).
Jumapili kutakuwa na mechi kati ya Stand United na Yanga (Kambarage),
na Ruvu Shooting na Toto Africans kwenye Uwanja wa Mlandizi mkoani
Pwani.
Kutokana na marekebisho
yanayofanyika Uwanja wa Uhuru, mechi ya kundi ya A ya Ligi Daraja la
Kwanza kati ya Ashanti United na Pamba iliyokuwa ichezwe Ijumaa,
Septemba 23 kwenye uwanja huo sasa itafanyika kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

0 Comments