Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.21,2016 SAA 11:18 JIONI
Mshambuliaji John Bocco wa Azam FC amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa
Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Agosti kwa
msimu wa 2016/2017.
Bocco ambaye pia ni nahodha wa Azam FC aliwashinda wachezaji Mzamiru
Yasin wa Simba na Said Kipao wa JKT Ruvu. Katika mechi mbili ilizocheza
katika mwezi huo, Bocco aliifungia timu yake mabao matatu likiwemo la
kusawazisha dhidi ya African Lyon.
Alifunga mabao mengine mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0 wa timu
yake dhidi ya Majimaji. Katika mechi hizo mbili, Azam FC ilifanikiwa
kupata pointi nne kati ya sita.
Mwezi huo ulikuwa na raundi mbili tu za Ligi hiyo iliyoanza kutimua
vumbi Agosti 20 mwaka huu. Kwa kushinda tuzo hiyo, Bocco atazawadiwa
kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni
ya Vodacom Tanzania.

0 Comments