Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:WACHEZAJI SERENGETI BOYS WAFUNGUKA NA KOCHA WAO JUU YA MECHI NA SHELISHELI

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 22,2016 SAA 02:48 USIKU
Kocha mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime akiendesha mazoezi
Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys wanaendelea na maandalizi ya kujiwinda na
mchezo wa mkondo wa kwanza wa kuwani nafasi ya kufuzu fainali za Afrika kwa vijana, dhidi ya timu ya taifa ya Shelisheli ambao umepangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakiwa kwenye hosteli za shirikisho la soka nchini TFF, ambapo ndipo Serengeti boys walipoweka kambi ya kujiandaa na mchezo huo, wachezaji wameonyesha kuwa tayari kupambana na kutimiza azma ya kujiweka katika mazingira mazuri kabla ya mchezo wa mkondo wa pili.

Nahodha wa kikosi cha Serengeti Boys Issa Abdi Makamba, amesema wanatambua lililo mbele yao ni zito na jambo hilo ndilo linawapa morari ya kufanya maandalizi kwa nguvu ili kuweza kuibuka na ushindi.

Mchezaji Shaban Zubeir Ado, amesema mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vyema na wanaamini michezo kadhaa ya kirafiki waliyocheza, itawasaidia kufikia lengo katika katika mtanange huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na watanzania wote.

Naye mshambuliaji yohana Oscar Mkomoya amesema anatarajia mchezo huo kuwa mgumu, lakini hawana namna zaidi ya kujiandaa kupambana na kujituma wakati wote.

SIKILIZA HAPA

WWakati huo huo kocha mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema hali ya kikosi chake inaendelea vyema na imekua ikiridhika siku hadi siku, hatua mbayo anaamini inaendelea kuwajenga wachezaji wake kisaikolojia kuelekea katika wimbi la ushindi.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments