Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Jamal Malinzi amempongeza mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na
klabu ya TP Mazembe ya Congo DR kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani.
Samatta ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wanaocheza Afrika baada ya kwashinda Robert Kidiaba (Congo DR) alieshika nafasi ya pili na Bounedjah Baghdad (Algeria) aliyeshika nafasi ya tatu.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Samatta amekua mchezaji wa kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki kushinda tuzo kubwa barani Afrika.
Pamoja na kushinda tuzo hiyo, Samatta pia amejumuishwa katika kikosi bora cha wachezaji wa Afrika kwa mwaka 2015 sambamba na Robert Kidiaba (Congo DR), Sergie Aurier (Ivory Coast), Aymen Abdenmor (Tunisia), Mohamed Meftah (Algeria), Sadio Mane (Senegal), Yaya Toure (Ivory Coast), Yacine Ibrahim (Algeria), Andrew Ayew (Ghana), Mbwana Samatta (Tanzania), Pierre-Emercik Aubameyang (Gabon) na Baghdad Bounedjah (Algeria).
Mshambuliaji Mbwana Samatta alieyambatana na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine wanatarajia kuwasili nchini leo saa 8 usiku kwa shirika la ndege la Ethiopia.
TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MOROCCO
Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa kocha msaidizi wa Taifa Stars Hemed Suleiman “Morocco” kufutia kifo cha baba yake mzazi Suleiman Ally Hemed kilichotokea juzi kisiwani Zanzibar.
Katika salamu hizo za rambirambi, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wapo pamoja na familia ya marheemu katika kipindi hiki kigumu cha maombeloezo.
Aidha pia TFF imetuma rambirambi (ubani) wa shilingi laki mbili (200,000) kwa familia ya kocha Hemed Moroco kufuatia kifo cha baba yake Suleiman Ally.
Mazishi ya marehmu Suleiman Ally Hemed mefanyika jana jioni mjini Zanzibar.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments