Uongozi wa klabu ya Simba imetoa msimamo wake kuhusiana na sarakasi za klabu ya Azam FC kupewa baraka na TFF za kushiriki
michuano maalum ya kimataifa iliyoanza rasmi hii leo mjini Ndola nchini Zambia.
michuano maalum ya kimataifa iliyoanza rasmi hii leo mjini Ndola nchini Zambia.
Uongozi wa klabu hiyo kongwe nchini, umetoka msimamo wake baada ya kamati ya utendaji kukutana jana na kujadili suala hilo ambalo limechukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari.
Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu Simba, Haji Sunday Manara amesema timu yao haitakubali kucheza mchezo wa mzunguuko wa 20 endapo timu zote hazitakuwa zimecheza idadi sawa ya mechi.
SIKILIZA HAPA
KKama hiyo haitoshi Manara amezungumzia namna walivyobaini kanuni za ligi zilivyovunjwa kwa makusudi na TFF pamoja na bodi ya ligi kwa lengo la kuinufaisha timu moja shiriki kwenye mshike mshike wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2015-16.
Amesema jambo lililofannywa na TFF haliwahi kufanyika miaka ya nyuma na kama lingetokea kufanyika basi Simba pekee walipaswa kufanya hivyo kutokana na uzoefu walioupata kwenye michuano ya kimataifa.
Hata hivyo Manara amesema barua watakayo waandikia TFF pamoja na bodi ya ligi wataianika hadharani ili watanzania wote wajue kinachoendelea pamoja na kutambua walichokiandika kwa maslahi ya kuona mchezo wa soka unachezwa kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa.
Amesema lengo lao kubwa kufanya hivyo ni hofu iliyojengeka dhidi yao kutokana na baadhi ya mambo yaliyowahi kujitokeza siku za nyuma ambapo maamuzi yake hayakurejeshwa Simba kama walalamikaji ama walalamikiwa.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments