Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS WA TFF JAMALI MALINZI KAZUNGUMZA JUU YA UCHAGUZI WA YANGA,AZAM KWENDA ZAMBIA NA MSIMAMO WAO JUU YA CHAMA CHA SOKA ZANZIBAR,taarifa kamili iko hapa...

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jan.28,2016 SAA 01:00 USIKU

1.Rais wa shirikisho la soka nchini TFF, Jamal Emil Malinzi amekubalia kubebesha mzigo wa lawama kufutia sakata la klabu ya
Azam FC kuruhusiwa kuelekea nchini Zambia katika mji wa Ndola, ili hali ratiba ya ligi ilikua haitoi nafasi kwa timu yoyote kuondoka katika kipindi hiki.

Malinzi amekubali kubebeshwa lawama za suala hilo, huku akiwaomba radhi wadau wa soka nchini waliokereka na maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya Azam FC ambao hawatocheza mchezo wao wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Tanzania Prisons.

Amesema kutokana na hali hiyo kujitokeza hakuna haja ya kumsaka mchawi zaidi ya kuangalia ni namna gani ambayo inaweza kusaidia kuziba viraka vya michezo itakayoihusu Azam Fc pindi itakaporejea nchini.

Hata hivyo Jamal Malinzi amechukua muda wake wa kukutana na vyombo vya habari hii leo, kuwafikishia ujumbe viongozi wa Azam FC, kuhusu mabadiliko yaratiba ya michezo ya ligi itakayowahusu mara baada ya kurejea nchini, huku akiwataka kukubaliana na changamoto ambazo zitawafika.

2.Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza msimamo wa kutoitambua kamati ya uongozi wa muda wa chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) na badala wanaendelea kuutambua uongozi ulio chini ya rais Ravia Idarous.

Msimamo huo wa TFF umewekwa hadharani na Jamal Malinzi alipozungumza na waandishi wa habari hii leo ambao walitaka kufahamu ipi nafasi ya Zanaibar katika soka la Tanzania, kufuatia mzozo ulioibuka jana bungeni.

3.Malinzi pia amelizungumzia suala la uchaguzi wa Dar es salaam Young Africans ambao umeibua sintofahamu kufuatia kauli iliyotolewa mwishoni mwa juma lililopita na mwenyekiti wa klabu hiyo Yousuph Mehboob Manji.
Epaphra Swai

4.Wakati huo huo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu, Epaphra Swai amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
TFF itawajulisha mipango ya msiba na mazishi ya marehemu Epaphra Swai baada ya kukaa na familia ya marehemu na kupanga utaraibu huo.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments