Ticker

6/recent/ticker-posts

HII NDIYO RATIBA YA LIGI KUU TZ BARA INAYOENDELEA JUMAMOSI HII

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jan.29,2016 SAA 10:00 JIONI
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja
tofauti, ikiwa katika mzunguko wa 16 kwa kila timu kusaka pointi 3 muhimu katika raundi hiyo ya lala salama.

Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi, Simba SC watawakaribisha African Sports, JKT Ruvu watawakaribisha Majimaji FC uwanja wa Karume, huku Mtibwa Sugar wakiwakaribisha Stand United kwenye uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Jijini Tanga, Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Young Africans uwanja wa Mkwakwani, Mwadui FC watakua wenyeji wa Toto Africans uwanja wa Mwadui Complex, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakicheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa mchezo mmoja ambapo Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribsiha Ndanda FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

MWILI WA SWAI KUSAFIRISHWA LEO

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linapenda kuwajulisha wapenzi, wadau, wa mpira wa miguu nchini kuwa, mwili wa aliyekua Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu, Epaphra Swai utaangwa leo saa 9 alasiri katika hosiptali ya Muhimbili, na baadae saa 11 jioni itaanza safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro.
Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu itafanyika leo Ijumaa saa 9 alasiri katika hospitali ya Muhimbili, ambapo ndugu, jamaaa, marafiki na wadau wa mpira wa miguu nwatapana nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Epaphra Swai, na baadae majira ya saa 11 jioni itaanza safari ya kuelekea Machame mkoani Kilimanjaro.
Mazishi ya marehemu Epaphra Swai yatafanyika kesho Jumamosi mchana nyumbani kwako Machame Kilimanjaro.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) inatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki, wadau wa mpira wa miguu pamoja na familia ya marehemu, na kusema wako pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo ya msiba huo.
Marehemu Epaphra Swai alifariki dunia jana asubuhi katika hospital ya taifa ya Muhimbili.


KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments