Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania imekiri kuheshimu na kufuata taratibu zilizowekwa na shirikisho la soka duniani FIFA
za kutotaka masuala ya soka kufikishwa mahakamani na badala yake vyombo vilivyounda ndani ya katiba za wanachama kuwa na mamlaka ya kutoa hukumu.
za kutotaka masuala ya soka kufikishwa mahakamani na badala yake vyombo vilivyounda ndani ya katiba za wanachama kuwa na mamlaka ya kutoa hukumu.
Naibu waziri wa habari, Utamaduini, Wasanii na michezo Annastazia James Wambura amelizungumza suala hilo bungeni hii leo, alipokua akijibu swali la mbunge wa jimbo la Konde, Khatib Said Hadji ambaye alitaka kufahamu ni kwa kiasi gani sheria za shirikisho la soka nchini za kutotaka masuala ya soka kufikishwa mahakamani, zinavyokinzana na sheria za nchi ya Tanzania.
Hata hivyo naibu waziri wa bahari, Utamaduini, Wasanii na michezo amesema bado serikali ipo katika mpango wa kuzifanyia marekebisho baadhi ya sheria za michezo ambazo zinainyima nafasi mchezo wa soka kutolewa maamuzi na mamlaka zinazotambuliwa na katiba za vyama vya soka.
SIKILIZA HAPA
JKatika hatua nyingine waziri wa habari, Utamaduini, Wasanii na michezo, Nape Nnauye, amelazimika kutolea ufafanuzi suala la mamlaka ya shirikisho la soka nchini kutokana na swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa jimbo la Konde, Khatib Said Hadji ambaye alitaka kujua TFF ina nafasi gani ndani ya chama cha soka visiwani Zanzibar.
Hata hivyo jambo hilo liliendelea kuchukua nafasi bungeni, baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, ambapo baadhi ya wabunge waliomba muongozi wa spika Job Ndugai, kwa kusema waziri wa habari, Utamaduini, Wasanii na michezo, Nape Nnauye ameupotosha umma walipokua akijibu swali la nyongeza.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments