Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Nov.14,2015 SAA 03:00 USIKU
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshindwa kuchomoza na ushindi baada ya kulazimishwa sare
ya kufungana magoli 2-2 na timu ya taifa ya Algferia kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Keita Mahamadou aliyesaidiwa na Diarra Bala na Niare Drissa Kamony wote wa Mali, hadi mapumziko tayari Tanzania walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Elias Maguri dakika ya 42 kwa kichwa akimalizia krosi beki Mwinyi Hajji Mngwali,Goli hilo likaipeleka Stars mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili, ni Taifa Stars tena iliyorejea uwanjani na moto na kufanikiwa kupata bao la mapema tu dakika ya 54, mfungaji Mbwana Samatta aliyemalizia pasi ya kiungo Mudathir Yahya Abbas.
Kwa upande wa Algeria Mabao yao Yote yalifungwa na mshambuliaji wake, Slimani Islam dakika ya 71 na 74.
Taifa Stars inatarajiwa kuondoka usiku wa manane leo kwa ndege ya Uturuki kwenda Algiers tayari kwa mchezo wa marudiano Jumanne.
ANGALIA PICHA ZA MCHEZO HUO
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments