Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:MASAA MACHACHE KABLA YA MECHI YA MARUDIANO YA TAIFA STARS,MANENO YAONGELEWA ,SIKILIZA HAPA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Nov.17,2015 SAA 02:00 USIKU
Mtihani wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wa kuendelea kuwa sehemu ya timu za Afrika zitakazowania kucheza fainali za
kombe la Dunia za mwaka 2018, utakamilishwa hii leo katika mji wa Blida nchini Algeria baada ya mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya awali dhidi ya wenyeji wao Mbweha wa jangwani.

Kikosi cha Stars ambacho kimeshawasili mjini Blida tangu juzi, kipo katika hali nzuri ya ushindani, kutokana na mwanzo mzuri wa matokeo ya sare waliyoyapata katika mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Algeria uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita jijini Dar es salaam.
Afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF, Baraka Kizuguto amesema mchezo wa  Stars dhidi ya Algeria umepangwa kuchezwa kuanzia mishale ya saa 1:15 jioni ambapo kwa hapa nyumbani itakua ni saa 3:15 usiku.

Haya hivyo Kizuguto amesema ari ya wachezaji wote ipo juu na wamedhamiria kupambana hadi dakika ya mwisho.

MSIKILIZE KIZUGUTO
 Lakini kumekuwa na hali ya kuweza kupoteza muda katika mechi kama hizi,kama ilivyokuwa katika uwanja wa taifa jijini dar es salaam.
Lakini kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa ameweza kuliongelea hilo kuelekea katika mchezo wa hii leo.

MSIKILIZE MKWASA

Lakini zile wanazoziita figisu figisu pia zimetokea huko nchini Algeria,baada ya hapo jana watanzania kulazimishwa kupanda gali la timu ya algeria,lakini watanzania hao waliweza kukataa kupanda gali hilo.

SIKILIZA HALI ILIVYOKUWA

Aliyekua mchezaji wa klabu ya Dar es salaam Young Africans Iddy Moshi, ameishauri kamati ya utendajhi ya shirikisho la soka nchini TFF kuwa na wigo mpana wa kusaka mbinu mbadala za kuisaidia timu ya Taifa ya Tanzania inapokua katika mtihani mzito kama walionao sasa wa kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

Iddy Moshi ambaye pia aliitumikia klabu ya Moro Utd, amesema kamati ya utendaji ya TFF imekua ikijisahau kusuka mbinu mbadala ambazo zitaweza kuleta tija katika harakati za kusaka namna ya kufaulu mitihani kwa timu ya taifa na badala yake imekua ikiunda kamati zisizokua na mashiko kwa kuangalia majina ya watu wakubwa tena wafanyabishara pekee.

Amesema hamaanishi kama kamati ya Taifa Stars inayoendelea na kazi kwa sasa inashindwa kufanya kazi yake ipasavyo, bali TFF kupitia kamati ya utendaji ilistahili kuwa na watu wa ufundi ambao pia wangeweza kutoa mchango wa mawazo ya kiufundi kuisaidia timu ambayo leo itakabiliwa na mchezo wa mkondo wa pili wa kuwani kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Algeria, huko mjini Algiers.

MSIKILIZE IDDI MOSHI


KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments