Ticker

6/recent/ticker-posts

TAARIFA YA TFF KUPIGA MARUFUKU SIASA IKO HAPA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.15,2015 SAA 02:27 USIKU

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limebaini kuwepo kwa vitendo vyaa wanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania
kujihusisha na masuala ya Siasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira ambayo yana nembo za vilabu na wadhamini wa Ligi.
Katiba ya TFF ibara ya I (4) inatamka “TFF is neutral in matters of politics and religion. Discrimination of any kind against a country, private person or group of people on account race, skin colour, ethnic, national or social origin, gender, language, religion, political opinion or any other opinion, wealth, birth or any other status is strictly prohibited and punishable by suspension or expulsion.”

Aidha kanuni za Ligi, Kanuni ya 14(40) inatamka: “ Hairuhusiwi kwa mchezaji, mwamuzi au kiongozi wa timu kuonyesha kwa njia yeyote tangazo au ujumbe unaohusiana na dini yeyote au ulio na madhumuni maalum bila idhini ya TFF/TPLB”.

TFF inachukua fursa kuwakumbusha wana familia wote wa mpira wakiwemo viongozi, wachezaji, waamuzi, makocha na madaktari wa michezo kuwa ni marufuku kuelezea hisia zao za kisiasa au kujihusisha katika kampeni za kisiasa wakiwa katika mavazi rasmi ya mpira zikiwemo jezi na track suites zenye nembo za TFF, vilabu wadhamini na ligi, Taifa stars au za washirika wa TFF wakiwemo wadhamini.
Mh.Mwigulu Nchemba ambaye ni Mwanasiasa akiingia uwanja wa taifa katika mchezo wa Yanga na Mtibwa Sugar ambapo mchezo huo Yanga ilishinda kwa mabao 2 - 0 Mapema mwezi wa 2 tarehe 8,2015
Aidha ni marufuku kwa mashabiki wa mpira kutumia fursa ya mechi za mpira wa miguu kubeba mabango au kusambaza ujumbe wa kisiasa.

Hatua kali zitachukuliwa kwa wataokiuka mahitaji ya katiba na kanuni za mashindano. TFF inatambua haki za wanamichezo kushiriki katika siasa ili mradi ushiriki wao hazikiuki kanuni na mahitaji ya katiba za TFF na FIFA.
 KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments