Manchester United ambao wamesubiri kwa muda kurudi kwao katika Ligi ya Mabingwa sasa watakuwa na kibarua
baada ya kusafiri kuwafuata mabingwa wa Uholanzi PSV Eindhoven leo Jumanne usiku.
baada ya kusafiri kuwafuata mabingwa wa Uholanzi PSV Eindhoven leo Jumanne usiku.
United mwisho wao kuonekana katika mashindano ya klabu za Ulaya ni Aprili 2014, baada ya kushindwa nafasi ya aina yoyote ya kushiriki mashindano ya Vilabu vya Ulaya msimu uliopita kufuatazo kumaliza nafasi ya saba msimu wa mwaka 2013/14.
Memphis Depay, aliyejiunga na Manchester United akitokea katika klabu ya PSV msimu huu, itakuwa na hisia juu ya kurudi kwake katika dimba la Philips, dhidi ya klabu yake ya zamani.
Wakati huo huo,kwa upande kocha wa PSV,Phillip Cocu akiingia katika mchezo wa leo akitarajiwa kuimalisha safu ya ulinzi baada ya kupokea kichapo cha mabao 6 - 0 kutoka katika klabu ya Cambuur,katika mchezo wa ligi ya Uholanzi.
Kapteni Wayne Rooney atakosa mchezo wa leo na Eindhoven kwa tatizo lile lile la kuumia, lililomuweka nje katika ushindi wa 3-1 siku ya Jumamosi dhidi ya Liverpool.
KOcha wa Manchester United Louis van Gaal amesema kwamba wataonyesha uwanjani kama wana uwezo wa kushinda mechi za ngazi ya juu, na akikiri kuwa Hiyo pia ni changamoto kwao kwa sasa,
lakini akisisitiza kuwa anahitaji ushindi katika mchezo wao wa kwanza ambao ni muhimu katika hatua ya makundi.
United watachezeza Mchezo wa Ligi ya mabingwa hii leo,baada ya Mwaka jana kumaliza katika nafasi ya nne katika Ligi Kuu.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments