Ticker

6/recent/ticker-posts

ANGALIA RATIBA VPL KESHO NA FDL

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.15,2015 SAA 10:23 JIONI
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea kesho jumatano katika viwanja saba nchini, huku timu 14
zikitarajiwa kuchuana kusaka pointi tatu muhimu katika michezo hiyo ya mzunguko wa pili.
Mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Young Africans watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Maafande wa Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa Simba SC katika dimba la uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Wana Lizombe Majimaji ya mjini Songea watawakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma, jijini Mbeya watoza kodi wa jiji timu ya Mbeya City Council FC watawakaribisha maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Ruvu katika uwanja wa Sokoine jijini humo.
Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Stand United watakuwa wenyeji wa timu ya Azam FC, Toto Africans watawakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Coastal Union kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Ligi hiyo itaendelea siku ya alhamis kwa mchezo mmoja tu kwa Wachimba Almasi wa mkoa wa Shinyanga, Mwadui FC watakapowakaribisha African Sports ya jijin Tanga katika mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Mwadui.
Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi Septemba 19 kwa michezo 10 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo jumla ya timu 24 zinashirki ligi hiyo ambayo washindi wa tatu watapanda ligi kuu ya Vodacom msimu ujao.
Kundi A, Polisi Dar watakuwa wenyeji wa Friends Rangers kwenye uwanja Mabatini mkoani Pwani, Mjii Mkuu ya Dodoma watapambana na  Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri mjini humo.
Kundi B, Polisi Morogoro watacheza na Burkina Faso uwanja wa Jamhuri Morogoro, Njombe Mji FC watacheza na Kurugenzi uwanja wa Amani mjini Njombe, Lipuli ya Iringa watawaribisha Kimondo FC uwanja wa Wambi- Iringa na JKT Mlale watakua wenyeji wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Kundi C, Mbao FC watawakaribisha Geita Gold uwanja wa CCM Kirumba, Rhino Rangers watacheza dhidi ya Polisi Tabora uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Panone FC watawakaribisha JKT Oljoro katika uwanja wa Ushirka mjini Moshi na Polisi Mara watakua wenyeji wa JKT Kanembwa kwenye uwanja wa Karume mkoani Mara.

Post a Comment

0 Comments