Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limepokea maombi ya klabu ya Young Africans (Yanga SC) ya kutaka kufanya
uchaguzi wake mkuu wa viongozi wa klabu hiyo kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya Utendaji.
TFF imeiomba klabu hiyo kufanya mkutano wake wa Uchaguzi wa viongozi baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Rais, Wabunge na Madiwani) utakaofanyika Oktoba 25, 2015.
Hii ni kutokana na unyeti wa uchaguzi wa klabu ya Yanga yenye matawi nchini kote.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

0 Comments