Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:NIGERIA WAJA TANZANIA NA KUMUULIZIA JUMA PONDAMALI...sikiliza...

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.4,2015 SAA 01:18 USIKU

Mwenyekiti wa umoja wa mashabiki wa timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Rafiu Ladipo wametamba timu yao itaibuka na
ushindi katikamchezo wa kesho ambao utakua na kusudio la kukusanya point zitakazowapeleka kwenye fainali za Afrika za mwaka 2017 ambazo zitachezwa nchini Gabon.

Ladipo ambaye amewasili nchini sambamba na kikosi cha mashabiki wa timu ya taifa ya Nigeria leo alfajiri amesema jukumu kubwa lililowaleta nchini ni kuhakikisha wanaisaidia timu yao kutimiza wajibu wa kuelekea kwenye fainali za mwaka 2017 na kwa jambo hilo hawatahitaji mzaha.

Amesema wamejitwisha jukumu hilo baada ya kupanda na hasira za kushindwa kushiriki fainali za Afrika zilizofanyika mapema mwaka huu nchini Equatorial Guinea kufuatia kikosi chao kufanya vibaya kwenye hatua ya kufuzu.
Juma Pondamali

Hata hivyo Rafiu Ladipo aliwashangaza waandishi wa habari pale alipomuulizia mlinda mlango wa zamani wa Taifa Stars Juma Pondamali ambae alikua langoni wakati fainali za Afrika za mwaka 1980.

Lapodo alifikia hatua ya kuwaomba waandishi wa habari kumshika mkono na kumpeleka alipo Juma Pondamali, kufutia hamu na shauku kubwa aliyonayo ya kutaka kumuona kocha huyo wa makipa wa klabu ya Dar es salaam Young Africans aliyokuwa nayo.

MSIKILIZE KIONGOZI WA MASHABIKI WA NIGERIA
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments