Baada ya kusubiri kwa muda wa miezi na majuma kadhaa, timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, kesho itakua na kibarua kigumu cha kuwakabili
mabingwa wa Afrika wa mwaka 1980, 1994 na 2013 timu ya taifa ya Nigeria katika mchezo wa kuwani kufuzu fainali za barani humo za mwaka 2017.
mabingwa wa Afrika wa mwaka 1980, 1994 na 2013 timu ya taifa ya Nigeria katika mchezo wa kuwani kufuzu fainali za barani humo za mwaka 2017.
Stars watakua nyumbani kwenye uwanja wa taifa chini ya kocha wao mzawa Charles Boniface Mkwasa wakihitaji kurejesha Imani kwa watanzania wote ambao walionyesha kuvunjika moyo wakati wa mchezo wa kwanza wa kuwani kufuzu kwenye fainali za Afrika dhidi ya timu ya taifa ya Misri ambayo iliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri ambapo wakati huo timu ya taifa ya Tanzania ilikua chini ya kocha kutoka nchini Uholanzi Mart Nooij.
Kocha wa timu ya taifa Stars Charles Boniface Mkwasa Master hii leo alizungumza na waandishi wa habari na kueleza namna alivyowaandaa wachezaji wa timu yao kuelekea katika mpambano huo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa.
Mkwasa pia alikumbushia mualiko wake kwa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alionyesha kukatishwa tamaa na mwenendo wa Taifa Stars na kufikia hatua ya kutangaza hadharani wakati akitoa hotuba ya kuvunja bunge mjini Dodoma July 09 mwaka huu.


0 Comments