Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers amepongeza kwa uchezaji wa mshambuliaji mpya Christian Benteke katika
ushindi dhidi ya Bournemouth siku ya jana usiku.
Benteke alifunga bao la kwanza na la pekee kwa klabu hiyo waliokuwa nyumbani na kuchomoka na ushindi wa bao 1-0.
"Nadhani alifanya maamuzi mengine katika mchezo, wakati timu inajaribu kufanya mashambuizi," alisema.
"Nilidhani uchezaji wake ulikuwa bora, Unaweza kuona miguu yake - alivyogusa nzuri na uelewa mkubwa, na bila shaka, kwa kawaida wakati mpira unakuja katika sanduku yeye alikuwa tishio kubwa"..
"Nilidhani alistahili bao lake na alisikitishwa kwa kutopata bao jingine. Lakini ilikuwa ni usiku nzuri kwake." alisema Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers
Wakiti huo huo Meneja wa klabu ya Bournemouth ya nchini Uingereza,Eddie Howe amesema maamuzi yaliyofanywa kinyume na matarajio ya wengi katika mchezo waliopoteza dhidi ya Liverpool hayasameheki.
Mapema mchezaji wa Bournemouth Tommy Elphick alikaribia kufunga lakini alinyimwa kwa kucheza vibaya.''Huwezi kupingana na maamuzi na mambo hayo yalitunyima alama muhimu'' alisema meneja wa Bournemouth mwenye miaka 37 Eddie Howe.
Howe alisema kuwa atajaribu kutizama nini kitafuatia kwa mwamuzi wa mchezo huo Craig Pawson pamoja na waaamuzi wasaidizi. Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Anfield,ambapo Liverpool waliondoka na ushindi mwembamba wa goli 1 kwa bila.
English Barclays Premier League | LOGS
| Pos | Team | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
| 1 | Manchester City | 2 | 2 | 0 | 0 | 6 | 0 | 6 | 6 |
| 2 | Leicester City | 2 | 2 | 0 | 0 | 6 | 3 | 3 | 6 |
| 3 | Liverpool | 2 | 2 | 0 | 0 | 2 | 0 | 2 | 6 |
| 4 | Manchester United | 2 | 2 | 0 | 0 | 2 | 0 | 2 | 6 |
| 5 | Everton | 2 | 1 | 1 | 0 | 5 | 2 | 3 | 4 |
| 6 | Swansea City | 2 | 1 | 1 | 0 | 4 | 2 | 2 | 4 |
| 7 | Crystal Palace | 2 | 1 | 0 | 1 | 4 | 3 | 1 | 3 |
| 8 | West Ham United | 2 | 1 | 0 | 1 | 3 | 2 | 1 | 3 |
| 9 | Norwich City | 2 | 1 | 0 | 1 | 4 | 4 | 0 | 3 |
| 10 | Aston Villa | 2 | 1 | 0 | 1 | 1 | 1 | 0 | 3 |
| 11 | Arsenal | 2 | 1 | 0 | 1 | 2 | 3 | -1 | 3 |
| 12 | Watford | 2 | 0 | 2 | 0 | 2 | 2 | 0 | 2 |
| 13 | Stoke City | 2 | 0 | 1 | 1 | 2 | 3 | -1 | 1 |
| 14 | Tottenham Hotspur | 2 | 0 | 1 | 1 | 2 | 3 | -1 | 1 |
| 15 | Newcastle United | 2 | 0 | 1 | 1 | 2 | 4 | -2 | 1 |
| 16 | Chelsea | 2 | 0 | 1 | 1 | 2 | 5 | -3 | 1 |
| 17 | Southampton | 2 | 0 | 1 | 1 | 2 | 5 | -3 | 1 |
| 18 | West Bromwich Albion | 2 | 0 | 1 | 1 | 0 | 3 | -3 | 1 |
| 19 | Bournemouth | 2 | 0 | 0 | 2 | 0 | 2 | -2 | 0 |
| 20 | Sunderland | 2 | 0 | 0 | 2 | 3 | 7 | -4 | 0 |
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

0 Comments