Waamuzi wa soka nchini wametakiwa kuwa na mazoea ya kutobweteka na mafanikio ya kupata beji ya shirikisho la soka
duniani FIFA, na badala yake wajizoeshe kwenda sambamba na kasi ya ushindani na waamuzi wengine duniani kote.
Ushauri huo kwa waamuzi wenye beji za FIFA umetolewa na rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Emil Malinzi, alipokua akifunga kozi ya waamuzi iliyokua ikifanyika jijini Dar es salaam kuelekea katika mshike mshike wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2015-16.
Malinzi amesema waamuzi wa Tanzania wanapaswa kuendana na vigezo vya kimataifa, ili kufanikisha azma ya kujiwekea historia ya kuchezesha michezo mingi zaidi duniani kupitia FIFA.
Malinzi pia ameendelea na kilio cha kutaka kupunguza kama si kutokomeza kabisa mchezo mchafu wa rushwa ambao umekua ukiklalamikiwa na baadhi ya wadau wa soka nchini japo hakuna ushahidi uliodhihiri mpaka sasa.
Malinzi amesema TFF inaendelea kupanga mikakati itakayosaidia kumaliza tatizo hilo hukua kitoa onyo kwa waamuzi waliohudhuria kwenye kozi hiyo kuacha kufikiria kujihusisha na masuala hayo machafu yanayopigwa vita ulimwenguni kote.
Naye mkufunzi wa kozi hiyo Soud Abdi ametoa shukurani kwa shirikisho al soka nchini TFF pamoja na kamati ya waamuzi kwa kuandaa darasa hilo kwa waamuzi ambapo anaamini litasiadia kuwakumbusha wahusika watakaopewa majukumu ya kusimamia sheria 17 za mchezo wa soka wakati wote wa msimu wa ligi kuu, ligi daraja la kwanza pamoja na ligi daraja la pili.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments