Ticker

6/recent/ticker-posts

LOUIS VAN GAAL ANATAKA KUSAJILI MCHEZAJI NYOTA,JE RONALDO KURUDI UNITED ? HIKI NDICHO ALICHOKISEMA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY.27,2015 SAA 12:25 JIONI

Louis van Gaal amesema anahitaji kumsajili mchezaji nyota kwa ajili ya kusaidia kufikia hamu yake ya kushinda taji la Ligi Kuu
kabla hajaondoka Manchester United katika miaka miwili.

Akizungumza na Sky Sports, Mholanzi huyo alikiri kwamba wakati umefika kwake kushinda taji la ligi, baada ya kutembea mbali na klabu hiyo, na chochote kinaweza kutokea.

Na kujipa nafasi kubwa ya kutambua hamu yake kwa Manchester United kushinda mataji manne ya Ulaya, Van Gaal anasema anahitaji kumsaini mchezaji kama Cristiano Ronaldo.

"Nadhani bado tunahitaji mwenye kasi zaidi pale mbele na pia ni awe na ubunifu zaidi na kwamba, nataka (Angel) Di Maria abaki, lakini hatujui kuwa kama tutakuwa naye na kumuona," alisema.

Lakini Louis van Gaal aliulizwa kama kuna uwezekano wa Ronaldo kurudi katika klabu hiyo kwa sasa?

"Siwezi kujibu maswali haya. Wakati sisi tunanunua mchezaji na yeye ana saini. Lakini hayuko katika mchakato na hayuko katika mkakati si wezi kusema hivyo" alisema.
" Nataka kusema hiki. Kwa mashabiki Nataka kusema hivi. Lakini siyo bora. Nina linda maslahi ya klabu."
Van Gaal hivi karibuni aligusia "kufanya usajili wa kustukiza" - anaweza kuwa na maana ya kurudi kwa Cristiano Ronaldo?

Hata hivyo  Louis van Gaal alimsifia Ronaldo akisema ni mchezaji mzuri na mchezaji huyo anajua kwamba anamvutia.
Tayari Manchester United imemsainisha kipa wa ArgentinaSergio Romero kwa mkataba wa miaka mitatu.
Kipa huyo mwenye miaka 28 anachukua nafasi ya mkongwe Victor Valdes aliyekosana na Kocha wake Luois van Gaal.
Romero aliwahi kucheza chini ya Van gaal katika timu ya AZ Alkmaar ya Uholanzi iliyotwaa ubingwa wa kombe la ligi ya Uholanzi mnamo mwaka wa 2009.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments