Ticker

6/recent/ticker-posts

ASTON VILLA WAMEMSAJILI MTOTO WA ABEDI PELE KAMA MBADALA WA CHRISTIAN BENTEKE

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY.28,2015 SAA 10:45 USIKU
New signing Jordan Ayew poses at the training ground
Aston Villa tayari wamemsajili mshambuliaji Jordan Ayew kutoka klabu ya Ufaransa Lorient.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23  alijiunga Villa kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada isiyojulikana, na inaaminika kuwa ni ya £ 12m, baada ya kufanikiwa kufuzu vipimo vyake vya afya.
Andre Ayew (kushoto) akishangilia goli lililofungwa na mdogo wake Jordan Ayew (kulia) wakati wakiichezea timu ya Olympique Marseille ilipocheza dhidi ya AC Ajaccio katika mechi ya Ligue 1, Ligi Kuu ya Ufaransa
Ayew anaungana wachezaji wenzake wa zamani wa Ligue 1 Jordan Amavi na Idrissa Gueye katika dimba la Villa Park, na mtoto huyo wa Abedi Pele,anaweza kujikuta anacheza dhidi ya ndugu Andre, ambaye amesaini katika klabu ya Swansea.
Abedi Pele (wa pili kutoka kushoto) akielekezwa jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto wakati akiwa katika ziara yake jijini Dar es Salaam. Wengine kulia ni Iddi Mshangana na , Henry Tandau.
Andre na Jordan Ayew ni wachezaji wa  timu ya taifa ya Ghana, Black Stars,na wamewahi pia kufundishwa na Kwesi Appiah ambaye sasa ni kocha wa timu ya Al Khartoum kutoka nchini Sudan,ambayo leo imeifunga APR ya Rwanda mabao 4 - 0 na kutinga hatua ya nusu fainali, ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) .
Jordan Ayew  ambaye ni Mshambuliaji wa zamani wa Marseille , alifunga mabao 12 katika mechi 26 za ligi akiwa na Lorient msimu uliopita na ameitwa mara 28  katika kikosi cha Ghana, atakuwa mbadala moja kwa moja wa Christian Benteke aliyehamia Liverpool kwa £ 32.5m.
"Najisikia radhi kwa kumleta Jordan katika klabu ," bosi wa Villa Tim Sherwood aliiambia tovuti  rasmi ya klabu hiyo.
"Yeye ni mchezaji kijana mzuri ambaye kikamilifu anafaa kwa Ligi Kuu."Tim Sherwood  alifafanua.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments