Ticker

6/recent/ticker-posts

KOCHA WA SIMBA KERR ATAMBULISHWA RASMI

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY.01,2015 SAA 01:13 USIKU
Kocha Kerr atambulishwa rasmi
Kocha mpya wa Simba sports club Dylan Kerr leo asubuhi ametambulishwa rasmi kwa wachezaji wa Simba kwenye
mazoezi yanayofanyika kwenye viwanja vya Sigara Chang’ombe.
Wachezaji waliohudhuria mazoezi hayo wameonyesha furaha kubwa kumpata kocha Kerr ambaye ameonesha kuwa ni kocha wa vitendo zaidi, kocha Kerr aliingia uwanjani na kuonesha kwa vitendo mafunzo yake.
Kocha huyo kutoka Nchini Uingereza ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika fani ya mpira wa miguu huku pia akiwa na umahiri wa kufundisha klabu mbalimbali duniani zikiwemo Hai Phong FC Vietnam, Hamilliton Academicals FC na Greennock Morton FC zote kutoka Scotland.
Kocha Kerr pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu za South Africa NFD Nathi Lions FC na  South Africa Thanda Royal Zulu FC kutoka Afrika Kusini
Kerr ana leseni ya daraja A na B ya ukocha aliyotunukiwa na Shirikisho la soka la Ulaya (UEFA) huku pia akiwa na uzoefu wa utawala katika fani ya michezo.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments