Ticker

6/recent/ticker-posts

HAMISI KIIZA AWASILI,KUFANYIWA VIPIMO

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY.02,2015 SAA 12:10 JIONI
Hamisi Kiiza awasili
Mchezaji Hamisi Kiiza ametua Dar es Salaam mchana huu akitokea nchini Uganda kwa ajili ya kufanya
vipimo vya afya na mambo yakienda vizuri kusaini mkataba wa kujiunga na Simba Sports Club. 


Taarifa kutoka katika tuvuti rasmi ya Simba inasema,Kiiza ametua Dar es Salaam akiongozana na mwenzake Simon Serunkuma ambaye amejiunga na Simba msimu uliopita.

Wakiwa uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere wachezaji hao wamesema wamekuja kwa ajili ya mapambano na kuhakikisha hadhi ya Simba inarudi. Alipozungumzia Simba Kiiza amesema anajua Simba ni timu kubwa sana barani Afrika kutokana na historia ya klabu hiyo na anajua wapenzi wa Simba wanahamu sana ya kumwona akichezea timu hiyo.
Hamis Kiiza ni mchezaji kutoka Uganda ambaye pia anacheza timu ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments