YANGA SC siku ya jana walizinduka katika michuano ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, maarufu
kama Kombe la Kagame, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Telecom ya Djibouti, katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
kama Kombe la Kagame, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Telecom ya Djibouti, katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo Tambwe alipiga nje mkwaju wa penalti dakika ya 39 baada ya winga Simon Msuva kuchezewa rafu kwenye boksi na Warsama Ibrahim Aden.
Warsama Ibrahim Aden akasababisha penalti nyingine, baada ya kuunawa mpira,penalti hiyo iliyopiga na Msuva dakika ya 43, tena ilipanguliwa na kipa Nzokira.
Beki wa klabu ya Yanga Nadir Haroub “Canavaro” ambaye pia alikosa Penalti katika siku za hivi karibuni,amezungumza na Jamii na Michezo juu ya Hali hiyo ya kukosa penalti kwa wachezaji wa Yanga.
MSIKILIZE NADIR HAROUB CANAVARO

0 Comments