Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY.27,2015 SAA 10:40 JIONI

Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu hii leo amezindua michuano ya Airtel Rising Star kwa mkoa wa Dare salaam, ambapo
timu kutoka wiliya za Ilala, Temeke na Kinondoni zinashikriki michuano hiyo.

Akifungua michuano hiyo, Zungu amewataka vijana kutumia vizuri nafasi hiyo ya michuano ya Airtel Rising kuonekana, kwani kutawapelekea kupata nafasi ya kucheza katika timu kubwa na kuweza kuendesha maisha yao kwa kupitia mpira wa miguu.

Mussa Zungu pia ameishukuru kampuni ya Airtel kwa kuendelea na mchakato huo wa kuibua vipaji,huku akivitaka vilabu vikubwa kutumia michuano hiyo kwa ajili ya kutafuta wachezaji watakaoisaidia Tanzania.



Kwa upande wa shirikisho la Soka Tanzania,Raisi Jamal Malinzi amewashukuru kampuni ya Airtel kwa kuibua vipaji mbalimbali,huku akiiomba kampuni hiyo kushirikisha mikoa mingi zaidi katika mashindano hayo.

Michuano ya Airtel Rising Stars imekua ikifanyika kila mwaka nchini kwa lengo la kusaka na kuibuka vipaji vya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, ambapo wachezaji wenye vipaji huchaguliwa na kupelekwa katika vituo vya kufundisha soka na wengine huchaguliwa katika kikosi cha Taifa cha Vijana (Serengeti U17).

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)