Ticker

6/recent/ticker-posts

SOLOMONI KOLOU AWALILIA AWALILIA ETO'O NA DROGBA

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Jan.20,2015 SAA 03:48 ASUBUHI
Mshambuliaji wa Ivory Coast Salomon Kalou amesema ni "vigumu kufikiria" Kombe la Mataifa ya Afrika bila wachezaji
wawili bora wa zamani wamashindano ya Afrika, Samuel Eto'o na Didier Drogba ..

Kalou, hata baada ya kushinikizwa kuwalinganisha nyota hao wawili wa Afrika na wale wa ulaya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, anahisi kwamba Cameroon na Ivory Coast - nchi mbili ambazo Eto'o na Drogba wanatoka, bado kuna baadhi ya majina mengine makubwa ya kuangazia katika mashindano ya AFCON nchini Equatorial Guinea.

Mshambuliaji huyo mwenye  mwenye umri wa miaka 29  anaamini kukosekana kwa Drogba na Eto'o hakutakuwa na athiri "kubwa" kwa Cameroon na Ivory Coast.
"Ndiyo ni kweli unaweza kuwaelezea kama wao," Kalou alisema Drogba na Eto'o katika mahojiano na Fifa.com kuwa  "Ni vigumu kufikiria. Lakini kidogo unaweza kujalibu kulinganisha miaka michache iliyopita, kufikiria Barca bila Ronaldinho na Real (Madrid) bila Zinedine Zidane, na bado leo tuna Messi na Ronaldo. Timu zote mbili daima wana wachezaji wapya wanaokuja na kuwa juu. Hata kama timu hizi mbili zitawakosa Didier na Samuel , mechi kati ya Ivory Coast na Cameroon daima ni kubwa na hii imekuwa kwa muda mrefu. Kuna ushindani mkubwa kati ya pande hizi na kwamba watakuwa juu, hata baada ya kustaafu kwa wachezaji hao mawili wakubwa. "
Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa Hertha Berlin alienda mbali zaidi kwa kusema Drogba na Eto'o, wao wana "mafanikio ya bara zima la Afrika."

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments