Raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imekamilika leo (Desemba 28 mwaka huu) kwa mechi tatu.
Macho na masikio ya watu wengi hii leo yalikuwa katika mchezo kati ya MABINGWA wa Tanzania Bara, Azam FC na Yanga SC,ambapo mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabingwa wa Bara, Azam FC watamshukuru mshambuliaji wao majeruhi wa muda mrefu, John Bocco ‘Adebayor’ambaye akicheza kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kutokea benchi, aliifungia timu hiyo bao la kusawazisha.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Mathew Akrama wa Mwanza, hadi mapumziko, tayari timu hizo zilikuwazimekwishafungana bao 1-1.
|
Kulia ni Kocha Hans van der Pluijm na Charles Boniface Mkwasa |
|
Benchi la Azama FC |
|
(katikati) KOCHA Mcameroon, Joseph Marius Omog akiwa na wasaidizi wake |
Azam FC walitangulia kupata bao kupitia kwa Mrundi, Didier Kavumbangu dakika ya tano akiupitia mpira uliotemwa na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ kufuatia krosi ya mshambuliaji wa Ivory Coast, Kipre Tchetche.
|
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao la kwanza |
Yanga SC wakasawazisha bao hilo dakika mbili baadaye kupitia kwa Mrundi pia, Amisi Tambwe aliyeunganisha kwa kichwa kwa krosi ya Salum Telela.
|
Mashabiki wa Yanga wakishangilia bao la kusawazisha |
|
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kusawazisha |
Kipindi cha pili, Yanga SC walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Simon Msuva dakika ya 51 akimalizia krosi ya Danny Mrwanda.
Mshambuliaji John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyetokea benchi kipindi cha pili alikwenda kuisawazishia Azam FC dakika ya 65, akimalizia krosi ya Himid Mao.
|
Mshabiki wa Yanga akitolewa katika jukwaa la Azam na kupelekwa katika Jukwaa la Yanga |
Matokeo haya, yanafanya timu hizo ziendelee kufungana kwa pointi 14 kila mmoja, baada ya mechi nane zikiwanyuma ya Mtibwa Sugar inayoongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 16.
|
Katikati ni Shabikia aliyejipatika Umaalufu kwa kulia uwanjani pale Yanga alipofungwa,sasa amehamishia mapenzi yake katika klabu ya Azam FC,(ANAJIITA STEVE AZAM) |
|
STEVE AZAM akiifurahia timu yake ya AZAM FC |
|
Wachezaji wakienda kupumzika baada ya dakika 45 za kwanza |
|
Mashabiki wa Azam FC wakichana Jezi ya mshabiki wa Yanga aliyekaa katika jukwaa lao |
|
Kocha Hans van der Pluijm akiingia uwanjani baada ya mapumziko |
|
Matokeo ya kipindi cha kwanza |
|
STEVE AZAM akiwa hana raha baada ya Yanza kupata bao la pili |
|
(Kushoto)STEVE AZAM akiwa hana raha baada ya Yanga kupata bao la pili |
|
Mashabiki wa Yanga wakimzomea Steve Azam |
|
STEVE AZAM alipata nguvu tena baada ya Azma FC kusawazisha bao la pili |
|
Mashabiki wa Azam FC wakishangaa baada ya mchezaji wao kukosa bao la wazi |
|
Wachezaji wa Azam na Yanga wakigombana uwanjani |
|
Matokeo ya mwisho wa mchezo |
|
Dakika tatu ziliongezwa |
|
Shabiki wa Yanga akiwa ahamini kama mpira unaelekea kumalizika na sare ya 2-2 |
Vikosi vilikuwa; Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Edward Charles/Oscar Joshua dk46, MbuyuTwite, Kevin Yondan, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe/Mrisho Ngassa dk75, KpahSherman na Danny Mrwanda/Hussein Javu dk73.
|
Kiungo mshamabuliaji Andrey Marcel Ferreira Coutinho raia wa Brazil leo hakucheza kabisa |
Azam FC; Mwadini Ali, Himid Mao/David Mwantika dk89, Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Serge Wawa, ErastoNyoni, Mudathir Yahya, Salum Abubakar/John Bocco dk64, Didier Kavumbangu, Kipre Tchetche na Brian Majwega.
|
Steve Azam akitupiana maneno na mashabiki wa Yanga baada ya sare ya 2 -2 |
|
Mashabiki wa Azam FC wakicheza baada ya mchezo kumalizika |
Mchezo mwingine katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya,Mbeya City imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1 - 0 dhidi ya timu ya Ndanda Fc kutoka Mtwara.
Mchezo wa Polisi Moro uliopigwa katika dimba la Jamuhuli Morogoro timu hiyo imechomoka na ushindi wa 2-0 dhidi ya timu ya Mgambo Jkt.
Nayo mechi kati ya Mtibwa Sugar na Stand United ambayo jana ilivunjwa na mvua dakika ya 6 imemaliziwa leo ambapo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Wakati huo huo, mechi ya ligi iliyochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex imemalizika kwa wageni Ruvu Shooting kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu. Bao hilo lilifungwa kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Hamisi Kasanga.
Ligi hiyo itaingia raundi ya tisa Januari 3 mwakani kwa mechi tano.
Coastal Union itacheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani, Ruvu Shooting itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Azam itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Azam Complex, Stand United itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati Mbeya City na Yanga zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Sokoine.
Ligi hiyo ambayo itachezwa mfululizo (non-stop) hadi itakapomalizika Mei 9 mwakani, itakamilisha raundi ya tisa Januari 4 mwakani kwa mechi kati ya Mgambo Shooting na Simba kwenye Uwanja wa Mkwakwani, na Tanzania Prisons itakayokuwa mwenyeji wa Ndanda kwenye Uwanja wa Sokoine.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments