Ticker

6/recent/ticker-posts

Hawa ndio wachezaji watatu watakaopambana katika Tuzo ya Ballon d'Or

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.DEC.01,2014 SAA 08:38 USIKU
Ni Ronaldo Na Messi Katika Tuzo Ya FIFA Ballon d
Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Manuel Neuer watakuwa wakipambana katika vita vya kuwania tuzo ya Ballon d'Or
kwa mwaka 2014 baada ya majina yao kutajwa katika orodha ya mwisho  kwa ajili ya tuzo hizo za kifahari.

Awali majina ya wachezaji 23 walitajwa - ambapo ni pamoja na Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale aliyekuwa mchezaji wa kipekee wa Uingereza kuorodheshwa kati ya wachezaji wanaoshindania tuzo hiyo ya mchezaji bora zaidi duniani Ballon d’Or.

Kwa sasa tuzo hiyo inashikiliwa na Cristiano Ronaldo baada ya kumbwaga mpinzani wake wa karibu Lionel Messi wakati wa hafla ya kutangazwa kwa mchezaji bora wa mwaka 2013 iliyofanyika mwanzoni mwa mwaka huu.  

Wawili hao wamewahi kutwaa tuzo ya mchezji bora zaidi ya mara moja ambapo kwa upande wa Lionel Messi aliwahi kuwa mshindi mwaka 2010, 2011 na 2012 ilihali Ronaldo alikuwa mshindi mwaka 2010 na 2013.

Orodha ya awali ya wachezaji 23 wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2014 iliyotolewa na FIFA.  

Gareth Bale (Wales, Real Madrid), Karim Benzema (France, Real Madrid), Diego Costa (Spain, Chelsea), Thibaut Courtois (Belgium, Chelsea), Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid), Angel Di Maria (Argentina, Manchester United), Mario Goetze (Germany, Bayern Munich), Eden Hazard (Belgium, Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Paris Saint Germain), Andres Iniesta (Spain, Barcelona), Toni Kroos (Germany, Real Madrid), Philipp Lahm (Germany, Bayern Munich), Javier Mascherano (Argentina, Barcelona), Lionel Messi (Argentina, Barcelona), Thomas Mueller (Germany, Bayern Munich), Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich), Neymar (Brazil, Barcelona), Paul Pogba (France, Juventus), Sergio Ramos (Spain, Real Madrid), Arjen Robben (Holland, Bayern Munich), James Rodriguez (Colombia, Real Madrid), Bastian Schweinsteiger (Germany, Bayern Munich) pamoja na Yaya Toure (Ivory Coast, Manchester City)

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments