Usajili wa wachezaji kwa dirisha dogo Tanzania kwa msimu wa mwaka 2014/2015 umefugwa rasmi juzi usiku huku
tukishuhudia vigogo wa soka Simba, Yanga pamoja na mabingwa watetezi Azam FC wakisajili nyota wengi wa kigeni.
Wekundu wa Msimbazi Simba Sc wamefanikiwa kufanya usajili wa wachezaji Hassan Kessy kutoka Mtibwa, Dan Sserunkuma ,Simon Sserunkuma, na Beki Juuko Murushid kutoka Uganda na kukamilisha idadi ya wachezaji watano toka Uganda akiwemo Joseph Owino na mshambuliaji Emmanuel Okwi.
KATIBU SIMBA:Stevin Ally
YANGA:
Kwa upande wa Yanga wao wamefanya marekebisho katika kikosi chao kwa kuwasajili Dany Mrwanda ,Kpah Sherman toka Aries Fc na Amisi Tambwe toka Simba Sc.
Pia kuna taarifa za kuachana na Bechi lao la ufundi akiwemo Kocha Marcio Maximo mara baada ya kufungwa na Simba katika mechi ya mtani jembe mabao 2-0.
AZAM Fc:
Mabingwa watetezi Azam Fc wamekamilisha usajili wa beki Serge Wawa Pascal kutoka Ivory Coast, aliyekuwa anacheza El Merreikh ya Sudan na Amri Kiemba aliyekuwa Simba SC, na winga Brian Majwega toka klabu ya Kcca,huku pia wakitangaza kuachana na mshambuliaji wa HAITI Leonal Saint-Preux kwa sababu ya kuwa majeraha.
Msemaji wa Azam Fc alithibitisha Swala hilo wakati akizungumza na Jamii na Michezo ,huku pia akitoa maelezo ya ziara ya timu hiyo ambayo iko Nchini Uganda kwa maandalizi ya Ligi kuu.
Na Vinara wa ligi hiyo Mtibwa Sugar wamewaongeza kiungo mzoefu Henry Joseph Shindika, na Abdul Jeba toka klabu ya Chuoni ya Zanzibar.
Kwa upande mwingine ni kwamba wachezaji 15 kutoka nje wakiombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kutoka nchi mbalimbali.
Wachezaji walioombewa ITC kwa timu za Ligi Kuu ni Abdulhalim Humoud kutoka Sofapaka ya Kenya kwenda Coastal Union, Brian Majwega kutoka KCC (Uganda) kwenda Azam, Castory Mumbara kutoka Three Star Club (Nepal) kwenda Polisi Mara, Charles Misheto kutoka SP Selbitiz (Ujerumani) kwenda Stand United na Chinedu Michael Nwankwoeze kutoka Nigeria kwenda Stand United.
Dan Serunkuma kutoka Gor Mahia (Kenya) kwenda Simba, Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Emerson De Oliveira Neves Roque kutoka Bonsucesso FC (Brasil) kwenda Yanga, Halidi Suleiman kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United na Juuko Murushid kutoka SC Victoria University (Uganda) kwenda Simba.
Kpah Sean Sherman kutoka Aries FC (Liberia) kwenda Yanga, Meshack Abel kutoka KCB (Kenya) kwenda Polisi Morogoro, Moussa Omar kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Nduwimana Michel kutoka Flambeau (Burundi) kwenda Stand United, Serge Pascal Wawa kutoka El Merreikh (Sudan) kwenda Azam na Simon Serunkuma kutoka Express FC (Uganda) kwenda Simba.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF inatarajia kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kupitia usajili wa wachezaji wote walioombewa katika dirisha dogo wakiwemo wale wa mkopo.
LIGI DARAJA LA KWANZA:
Kwa upande wa Ligi daraja la kwanza timu ya Mwadui Fc chini ya kocha Jamuhuri Kihwelo wamefanya usajili wa Beki wa Simba Joram Mgeveke na kusema kuwa Razima warudi Ligi kuu Msimu ujao.
Tayari timu hiyo imeshawasajili Razak Khalfani,Mohamed Mkweche na Uhuru Selemani na kocha Kihwelo amesisitiza kuwa Nidhamu ni muhimu kwa kikosi chake.
Jamuhuli Kihwelo amezungumza na Jamii na Michezo na ambapo pia amewataja wachezaji aliowaacha katika kikosi chake.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments