Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema ana nia ya kuwafunga Schalke 04 usiku wa leo jumanne ili kuepuka
kuzuiwa kufuzu katika hatua ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa UEFA chini ya duru la mwisho la mechi.
Chelsea imesafiri hadi nchini ujerumani ikiwa inaongoza kundi lao G na Schalke  wana  pointi tatu nyuma ya Timu hiyo ya London Maghalibi.
"Tuna cheza mechi nyingi mwezi Desemba hivyo ni bora kama tunaweza kuhitimu na kuepuka  shinikizo. Ni wazi kwamba itakuwa nzuri sana  kwetu,lakini Ukweli ni kwamba tunahitaji pointi,na sisi tutajaribu kufanya hivyo kesho(Leo).alisema Jose Mourinho
 kabla ya mechi akiwa katika mkutano wake na vyombo vya habari Mourinho pia aliulizwa na mwandishi wa habari wa Ujerumani juu ya matarajio yake,wakatia anakabiliwa na mchezaji wa Zamani wa Chelsea na meneja Roberto Di Matteo.
Yeye alijibu: "Mimi sipo hapa kusema kuhusu Di Matteo. Mimi niko hapa kuzungumza kuhusu mchezo. Kama unataka kufanya hivyo mimi niko tayari. "Mourinho alimalizia.
MECHI ZINGINE ZA LEO 
 
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 
 
0 Comments