Ticker

6/recent/ticker-posts

SOMA ALICHOKISEMA ROY HODGSON BAADA YA USHINDI DHIDI YA SWITZERLAND

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Sept.09,2014 SAA 09:46 USIKU
Roy Hodgson anaamini kuwa England 'imekuwa ikijengeka' kutokana na aina ya uchezaji wao,na hayo ameyasema mara
baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi Uswisi siku ya  jana Jumatatu.

Simba hao wa Tatu walifungua kampeni zao za michuano ya kufuzu kombe la ulaya 2016 kwa ushindi wa pointi tatu za kuvutia kutokana na mabao mawili ya Danny Welbeck.

Hodgson anasisitiza kuwa kamwe haulizi kwa nini inawezekana?, hata baada ya kukatishwa tamaa katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil, kwa kikosi chake cha vijana, bado ana kazi katika mipango yake ya michuano ya Ulaya 2016 nchini Ufaransa.

Aliwaambia Sky Sports: "Nadhani kila ushinda ni muhimu na kila mchezo kama meneja wa England ni muhimu".

"Nakubaliana kwamba mchezo huu ulikuwa una umuhimu wa kipekee kwa sababu sisi tunahitajika kucheza vizuri na kupata matokeo mazuri dhidi ya timu,ili tuwe katika nafasi ya juu katika viwango kuliko tulipokuwa wakati huu".
"itabidi kufanya hivyo, na tutaweza kufurahi katika hilo, lakini kwa upande mwingine, narudia tena kusema, nadhani tumekuwa tukijenga aina hii ya uchezaji katika kipindi cha miaka miwili".
"Tumekuwa tukibadilisha timu yetu na wachezaji zaidi ya miaka miwili. Tulikuwa na bahati mbaya nchini Brazil, lakini hatukuwa na maendeleo mabaya.Tuna uwezo wa kurudi juu, kuimalisha maendeleo  yetu, kuwarudisha nyuma, na  sisi kwenda tena. "alisema Roy Hodgson 

KWA TAARIFA,MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,BREAKING NEWS,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments