Katibu mkuu wa baraza za la michezo nchini Tanzania Henry Lihaya amekabihi bendela kwa timu ya taifa ya mpira wa magongo
kwa upande wa wanawake na wanaume wanaokwenda kuwakirisha nchi ya Tanzania katika mashindano ya kufuzu raundi ya kwanza ya kombe la dunia ya mchezo wa mpira wa magongo yanayotarajiwa kuanza tarehe 5 na kumalizika tarehe 8 mwezi wa tisa.
kwa upande wa wanawake na wanaume wanaokwenda kuwakirisha nchi ya Tanzania katika mashindano ya kufuzu raundi ya kwanza ya kombe la dunia ya mchezo wa mpira wa magongo yanayotarajiwa kuanza tarehe 5 na kumalizika tarehe 8 mwezi wa tisa.
Kocha wa timu ya wanawake valentina.quaranta akizungumza |
kikosi hiko cha wawakilishi wa Tanzania wanatarajiwa kuanza safari tarehe 1 mwezi wa tisa na kufika tarehe hiyo hiyo usiku.
Akizungumza na wanamichezo hao wakati wa kukabidhi bendera ya Taifa Katibu mkuu wa baraza za la michezo nchini Tanzania Henry Lihaya amekipongeza chama cha mchezo huo kwa ajili ya maandalizi waliyofanya ikiwemo kutafuta wadhamini ambao ni takribani 11 waliojitokeza kudhamini timu hiyo,lakini amewatakia wanamichezo hao mashindano mema na kuwataka wakumbuke kuwa watanzania wote wanategemea ushindi.
Focus Poul (KUSOTO) akikabidhiwa bendera kwa niaba ya timu ya wanaume |
Naye nahodha wa timu ya taifa ya mpira wa magogo kwa wanaume Focus Poul amesema wamepata maandalizi ya kutosha,kwa hiyo watanzania wategemee mambo mazuri na kuwataka watanzania walioko kenya kujitokeza kwa ajili ya kuunga mkono.
Kidawa Selemani (KULIA) akikabidhiwa bendera kwa upande wa wanawake |
Naye Nahodha kwa upande wa wanawake Kidawa Selemani amesema wachezaji wote wanamolari ya kutosha na kujinasibu kuwa wataibuka na ushindi kwa kuwa wamefanya mazoezi ya kutosha kwa kucheza na timu za wanaume kwa ajili ya kujijenga vizuri katika mashindano hayo.
Jamii na Michezo imekuandalia makala kwa ajili ya kufahamu changamoto za wachezaji wa mchezo huo wakati wa maandalizi yao kwa ajili ya mashindano hayo,unaweza kusikiliza kwa njia ya Audio au katazama kwa njia ya Video.
VIDEO:
AUDIO:
WACHEZAJI WATAKAO WAKILISHA NCHI KWA UPANDE WA WANAUME
0 Comments