huo utazinduliwa tarehe 8 Mwezi wa kumi mwaka huu,siku ambayo Tanzania itakuwa ikisheherekea miaka 50 ya kujiunga na FIFA.
Akizungumzana na waandishi wa habari katika ufungaji wa mafunzo ya wiki mbili ya makocha wa mpira wa miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) jijini Dar es Salaamn jana (Juni 20 mwaka huu), Rais Malinzi amesema watanzania wanatakiwa kujua kuwa bila kuwekeza katika mpira wa vijana wadogo,kamwe hatutaweza kushiriki kombe la dunia.
"Tanzania tulijiunga na FIFA tarehe 8 mwezi wa 10 mwaka 1964,na mzee Blatter Rais wa FIFA nimeshamuelezea kuhusu siku hiyo, na ameniahidi kwamba atatuma ujumbe mzito hapa nchini kushuhudia uzinduzi wa hiyo Program,bila shaka na wenzetu wa CAF watatuma ujumbe siku hiyo"alisema Malinzi
Malinzi ameongeza kuwa,katika mpango huo Tff lazima wafanye jitihada kuhakikisha kuwa kila shule ya msingi kwa hapa Tanzania kwa mwaka angalau inapata mipira 10 na jezi na viatu angalau 30.
“Kila mwaka tutakuwa na mashindano ya kitaifa ya watoto wenye umri chini ya miaka 13 kuanzia mwaka huu,tutakuwa tunateuwa vijana wazuri kulingana na mashindano hayo bara na visiwani, na hao vijana watakuwa wanahamishwa kutoka katika shule zao wanakwenda kuishi katika Academy,Hivyo ninyi makocha huko mnaporudi muwafundishe walimu wa shule za msingi mafunzo ya awali ya ukocha,” alisema.
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments