IMEWEKWA.Jun. 21,2014 SAA 10:36 JIONI
Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Bw Yusuf Manji amesema wanachama wanaopinga maamuzi ya mkutano
mkuu uliofanyika Juni Mosi 2014 katika Bwalo la Polisi Osyterbay ya kuwaongezea muda wa mwaka mmoja, wafike makao makuu ya klabu na kujiorodhesha majina yao kwa Katibu Mkuu.
mkuu uliofanyika Juni Mosi 2014 katika Bwalo la Polisi Osyterbay ya kuwaongezea muda wa mwaka mmoja, wafike makao makuu ya klabu na kujiorodhesha majina yao kwa Katibu Mkuu.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, Manji amesema sisi sote tunajenga nyumba hatuna haja ya kugombania fito, wanaopinga maamuzi yale ni vyema wakajiorodhesha majina yao ili kuweza kupata idadi yao na kama itafikia idadi ya waliohudhuria mkutano ule watu 1522 basi tutaitisha mkutano mwingine.
Zoezi la kujiorodhesha wanachama makao makuu litakua na usalama wa kutosha kutoka kwa jeshi la Polisi ambapo patakua na askari wa usalama watakao kuwa wakilinda usalama wa wanachama wanaofika kujiorodhesha kwenye reja hiyo.
SIKILIZA MAONGEZI YOTE YA MANJI KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI LEO
USISAHAU KULIKE PAGE YA FACEBOOK, BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments