Ticker

6/recent/ticker-posts

FIFA WATUA TANZANIA, KATIBU MKUU JEROME VALCKE ASHINDWA KUJA,SABABU IKO HAPA

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 01,2014 SAA 05:10 USIKU
Semina ya mawasiliano kwa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA) imefunguliwa leo May 1 na Nicholas Maignot ambaye ni naibu wa maswala ya mawasiliano kutoka FIFA.
Nicholas Maignot
Semina hiyo iliyoandaliwa na FIFA itafanyika kwa siku mbili (Mei 1 na 2 mwaka huu) na washiriki wa semina hiyo ni marais, makatibu wakuu na wakuu wa mawasiliano wa wanachama 12 wa CECAFA ambao ni Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somali, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.

Semina ikiendelea
KUTOKA KULIA NI:Zelkifli Ngoufonja ni misimamizi wa maendeleo ya soka la Afrika.Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania,Nicholas Maignot ambaye ni naibu wa maswala ya mawasiliano kutoka FIFA,Leodegar Tenga ambaye ni Mwenyekiti wa CECAFA na Emmanuel Maradas ambaye ni mshauri wa maswala ya habari

Awali semina hiyo ilitakiwa ifunguliwe na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Jerome Valcke,lakini kwa sababu za kifamilia ikalazimika amtume muwakilishi wake aweze kumuwakilisha.

Jerome Valcke
Mke Jerome Valcke amejifungua mtoto siku ya jana aliyepewa jina la Valent,hivyo kumfanya kiongozi huyo wa juu kabisa katika mchezo wa soka Duniani kusitisha majukumu yake ya shirikisho na kuweza kukaa karibu na mkewe.

Post a Comment

0 Comments