Ticker

6/recent/ticker-posts

European Qualifiers: mchezaji wa Manchester United Daley Blind anakabiliwa na maumivu

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.NOV.18,2014 SAA 12:43 ASUBUHI
Kiungo wa Manchester United Daley Blind anasumbuliwa na maumivu ya goti  aliyoyapata katika mchezo katika ambao
Holland ilishinda mabao 6-0 dhidi ya Latvia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 , ambaye alijiunga na United kutoka klabu ya Ajax katika majira ya joto,alikumbana na changamoto na mchezaji Eduards Visnakovs katika dakika ya 20, na klabu ya machester United watakuwa wanasubiri matokeo vya uchunguzi siku ya Jumatatu.

Meneja Guus Hiddink alitoa tathmini mbaya ya kuumia alipoulizwa kuhusu Blind kufuatia filimbi ya mwisho  kulia katika dimba la Amsterdam.

"Mimi sio daktari, lakini kesho anakwenda kufanyiwa vipimo,sina matarajio mazuri,Nadhani vipimo vya maabala vinaendelea,sijui lakini anaweza kuwa kapasuka au la,sijui"alisema kocha  Guus Hiddink
Blind  mwenyewe baadaye aliweka ujumbe katika akaunti yake ya  Instagram:akisema kuwa "najiikia fahari kucheza mechi yangu ya 25 na timu ya taifa ya Uholanzi, lakini ndio hivyo tena nimeuumia mguu wangu ...  itabidi nikae pembeni (na) nitarejea kwa nguvu, Hata hivyo tumeshinda ushindi mkubwa wa  mabao 6-0! "alisema Daley Blind

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments