Chelsea wako katika mawindo baada ya kuvamia academy ya Barcelona na kumsajili winga Josi Quintero.
Kijana huyo mwenye kipaji ambaye ana umri wa miaka 17, yeye mwenyewe ndiye aliyefichua siri hiyo baada ya kuweka picha katika akaunti yake ya Twitter akimwaga wino katika karatasi na kisha kutupia Jezi ya klabu hiyo, na kuambatanisha na maneno 'furaha kusaini mkataba wangu wa kwanza wa mchezaji wa kulipwa na klabu hii kubwa".
Talent: Josi Quintero puts pen to paper on his deal with Chelsea
Chelsea walikuwa na mawazo ya kuwa na mchezaji huyo ambaye amekuwa akizivutia pia klabu kama Arsenal na Lyon Lakini Quintero ilitangaza wiki iliyopita kuwa alikuwa ameshikilia mazungumzo yake na Chelsea na sasa uhamisho ndiyo umekamilika huku akiwa katika mafunzo na klabu hiyo tangu Januari.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ekuador ilikuwa kwenye benchi katika mchezo wa kirafiki wa Chelsea chini ya miaka 21 dhidi ya Sutton United siku ya Jumamosi.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments