Ticker

6/recent/ticker-posts

JOSE MOURINHO ATHIBITISHA KUSAJILI WACHEZAJI WAWILI WAKUBWA,JE NI DIEGO COSTA?

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 02,2014 SAA 04:06 USIKU
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amekiri kuwa anatazamia kuwasaini wachezaji wawili wakubwa msimu huu - lakini
amekataa kuthibitisha juu ya Diego Costa.

Costa ambaye ni Mshambuliaji  Atletico Madrid na Hispania alionesha mchezo mzuri katika  Ligi ya Mabingwa na kuwatoa the Blues katika nusu fainali mapema wiki hii na kuna uvumi Mourinho ana nia ya kumuongeza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 katika kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.

Lakini wakati Mourinho akithibitisha kuwa amevutiwa kumleta angalau mshambuliaji mmoja wa daraja la juu  ndani ya Stamford Bridge katika kipindi cha dirisha la uhamisho , alikatisha kujadili malengo yake maalum kwa yoyote yule.

Alisema kwa Kireno: "Kitu kimoja tu nasema ni kwamba dirisha limefungwa,likifunguliwa  tutajua katika majira ya joto".

"Chelsea itakuwa shwari kabisa na utulivu katika kipindi hicho. Timu Haiwezi kuwa na  kelele  za kuuza na kununua, kununua na kuuza, sisi si aina hiyo ya klabu".

"Tuta kwenda kujadili, napenda kusema, tutasaini wachezaji wawili muhimu. Je,ni mshambuliaji ambaye tunamlenga? Ndiyo. Je,ni Diego (Costa) mchezaji mzuri? Ndiyo,lakini yeye ni mchezaji wa Atletico Madrid  hivyo siwezi kusema sana. "

Mourinho amesababisha utata mapema wiki hii, zilipotoka siri kuwa anampango wa kuwatema Fernando Torres, Samuel Eto'o na Demba Ba katika kipindi cha uhamisho.

Mourinho ana ujasiri kuwa Chelsea itakuwa katika nafasi nzuri ya  kushinda kombe la ligi msimu ujao baada ya 'msimu wa mpito' katika uwanja wa Stamford Bridge.

Post a Comment

0 Comments