Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 06,2014 SAA 11:00 ALFAJIRI
Brendan Rodgers amekubali kushindwa katika mbio za
kugombea ubingwa wa ligi kuu kufuatia Liverpool kutoka sare na Crystal Palace.
Liverpool walikuwa wakiongoza kwa mabao 3-0 katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Selhurst Park jijini London na walikuwa wakijiamini wangeondoka na faida ya alama tatu ambazo zingewaweka mbali kidogo na Manchester City.
Liverpool sasa wampanda kileleni baada ya kufikisha pointi 81, huku Manchester City wenye michezo miwili mkononi wakiwa nafasi ya pili kwa pointi 80.
Majogoo hao wa jiji walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 18 kipindi cha kwanza kupitia kwa Joe Allen, dakika ya 53 Daniel Sturridge akifunga bao la pili,na bao la tatu lilifungwa dakika mbili baadaye na Luis Suarez ambaye aliishiwa nguvu na kububujikwa na machozi baada ya mchezo kumalizika asiamini kilichotokea.
Na mabao ya Crystal Palace yalifungwa katika dakika ya 79 na Damien Delaney, na
Dwight Gayle ambaye alifunga mabao mawili dakika ya 81 na dakika ya 88 na mechi kuisha kwa sare ya 3-3.
Alipoulizwa kuhusu kokosa ubingwa msimu huu kwa timu hiyo yenye ukame wa miaka 24 bila kikombe, Rodgers aliiambia Sky Sports: "Ndiyo, nadhani tulihitaji kushinda usiku wa leo ili kuweka pressure kubwa"
"Manchester City, wao wana michezo miwili nyumbani sasa, michezo miwili mgumu, lakini sisi tulihitajika kushinda. Nadhani Manchester City wata kwenda juu na kushinda michezo yao mawili na watakuwa mabingwa".
"Lakini kwa sisi kumekuwa na msimu bora hadi sasa. Kwa upande wetu kupata pointi 81 ni mafanikio makubwa, ni wazi tumesikitishwa,lakini tutaweza kufanya tena".
"Tunamchezo mkubwa katika uwanja wa Anfield sasa, tunamaliza msimu na tutaweza kuendelea kutafuta katika kujenga na kuendeleza kile tunachokifanya."
Rodgers anakubali kwamba Liverpool watajilaumu wenyewe kwa makosa machache dhidi Palace, na uwezo wa kukosa kuona mapungufu kwa haraka ndicho kilichoighaimu tumu hiyo.











CRYSTAL PALACE Speroni 6; Mariappa 6, Delaney 7, Dann 6.5, Ward 6.5; Jedinak 5.5, Dikgacoi 5; Bolasie 7, Ledley 6, Puncheon 5 (Gayle 65, 7); Chamakh 5 (Murray 71, 6).
Booked: Dann, Mariappa.
Goals: Delaney 79, Gayle 81, 88
Manager: Tony Pulis 7.
LIVERPOOL Mignolet 6; Johnson 6, Skrtel 5.5, Sakho 5.5, Flanagan 6; Gerrard 6, Allen 7, Lucas 5.5; Sterling 7 (Coutinho 78, 6), Suarez 8, Sturridge 7.
Booked: Allen, Suarez, Skrtel.
Goals: Allen 18, Sturridge 53, Suarez 55
Manager: Brendan Rodgers 6.
Referee: Mark Clattenburg 7.
0 Comments