Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.May. 01,2014 SAA 10:06 ALFAJIRI
Bosi wa Chelsea Jose Mourinho alikataa kuikosoa timu yake baada ya kutolewa nje ya Ligi ya Mabingwa ulaya katika
nusu fainali ya pili dhidi ya Atlético Madrid, kwa kupoteza kwa mabao 3-1 katika uwanja wa Stamford Bridge.
The Blues walikuwa mbele kwa kufunga bao la katika dakika ya 36 kupitia kwa mchezaji wa zamani wa Atlético Madrid Fernando Torres ambaye hakushangilia bao hilo, lakini hawakuweza hutegemea kama Adrian Lopez angeweza kupangua bao hilo dakika moja kabla ya kwenda mapumziko .
Ndani ya dakika 60 ya mchezo Ateltico ilipata bao lingine kwa mkwaju wa penalti ambayo ilipigwa Diego Costa.
Arda Turan alifunga bao la tatu dakika ya 72 , na Mourinho anakubali kwamba timu yake hakuweza kushinda kutokana na mambo mengi zaidi - lakini alijisifia kuwa walikuwa na timu bora mpaka pale Atletico walipotangulia".
"Nadhani mpaka penalti hawakuwa na timu bora," aliiambia Sky Sports.
"Tuli cheza, tulimiliki zaidi, nafasi zaidi, sisi tulifunga bao kubwa - tulikubali kufungwa mabao mepesi- tulijua tunajiweka katika vipande vipande huku tukitaka kuwa na nafasi".
"Terry alikuwa na nafasi kubwa lakini ilikuwa ni ajabu kuokoa, na baada ya hapo kukawa na penalti ya kuuawa mchezo na kulikuwa na timu moja tu ndani. Tulikuwa tukijaribu na wachezaji walikuwa wakijaribu kila kitu,lakini tangu wakati huo ukweli ni kwamba tulijua tumepoteza mchezo kwa sababu ya wakati mgumu wa wachezaji."
Licha ya yote hayo Mourinho amekubali matokeo, na amewapongeza Atlético Madrid kwa kufika fainali itakayopigwa May 24 mjini Lisbon nchini Ureno, lakini anaamini timu zote mbili za Madridi zina nafasi ya kushinda taji hilo Huku akiomba radhi kwa walipofikia Chelsea msimu huu, lakini akatabiri kuwa msimu ujao utakuwa bora zaidi ya msimu huu kwa kikosi chake.
Real Madrid nao wamefanikiwa kufika fainali ambapo sasa watacheza na Atlético Madrid, baada kuifunga Bayern Munich kwa 4-0 mjini Munich na kufanya ushindi wa jumla wa 5-0.
0 Comments