Ticker

6/recent/ticker-posts

NBA:MMILIKI WA LOS ANGELES CLIPPERS DONALD STERLING AFUNGIWA MAISHA KWA UBAGUZI WA RANGI,NA TIMU IKO KATIKA HATIHATI YA

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 30,2014 SAA 04:48 ASUBUHI
Donald Sterling: Banned for life
Mmiliki wa klabu ya mpira wa kikapu ya Los Angeles CLIPPERS kutoka marekani , Donald Sterling amefungiwa
maisha kujihusisha na mchezo huo na kupigwa faini kubwa na shirikisho la mpira wa kikapu nchini humo (NBA) baada ya maneno yake ya ubaguzi wa rangi yaliyonaswa hivi karibuni.

Kamishna wa NBA Adam Silver aliwaambia waandishi wa habari kwamba Sterling alipigwa faini ya $ 2.5m na kusimamishwa katika ligi hiyo maisha kutokana na kashfa hiyo - ambayo alimwambia mpenzi wake kuwa hataki  kumuona hadharani na wenzake wamarekani weusi katika michezo ya CLIPPERS.

Maoni Sterlings yalisababisha hasira katika nchi ya Marekani na nyota kadhaa wa NBA,pamoja na Rais Barack Obama ambaye ali laani kitendo hiko.

Silver  alisema kuwa : "maoni yaliyotolewa na Mr Sterling yana kera sana na yameleta madhara, Hivyo yamefika kwa wamiliki wa NBA kwani yameongeza hasira na kwangu pia".
"Sisi tunasimama pamoja kulaani maoni ya Mr Sterling . Kwa kifupi watu kama yeye hawana nafasi katika NBA.
Silver alisema Sterling alikiri kuwa ilikuwa ni sauti yake ambayo ili rekodiwa, na kuwekwa kwenye tovuti TMZ mwishoni mwa wiki.
Sterling mara moja amezuiliwa kuhudhuria michezo yoyote ya NBA au mazoezi, na kuiwakilisha CLIPPERS kivyovyote iwe kiofisi , kushiriki katika biashara au maamuzi yeyote kwa wachezaji na wafanyakazi wanaohusiana na timu.
Pia hawawezi kushiriki katika biashara yoyote ya ligi kuanzia sasa.


Silver alisema kuwa, amewaomba wamiliki wa NBA na mamlaka yao kumshinikiza Sterling kuuza timu, ambayo ina thamani ya $575 million kulingana na Forbes magazine .

Sterling alinunuliwa klabu hiyo mwaka 1981 kwa $12 million.
Wachezaji wa Los Angeles Clippers, walifanya mazoezi yao ya kujiandaa kwa mechi siku ya Jumapili wakiwa wamevalia jezi zao ndani nje ili kuficha nembo ya timu hio.

Bwana Sterling aliambia mtandao wa TMZ kwamba matamshi hayo hayakuwa ishara ya msimamo wake.

Clippers walikuwa wanacheza dhidi ya Golden State Warriors mjini in Oakland Jumapili. Katika mechi muhimu ya NBA, iliyozingirwa gumzo kuhusu hoja ya matamshi ya bwana Donald Sterling mwenye umri wa miaka 80 yaliyorekodiwa kisiri.

Wachezaji hao pia walivalia mikanda mieusi na soksi nyeusi pamoja na jesi zao za kawaida.

Post a Comment

0 Comments