Ticker

6/recent/ticker-posts

LIGI YA MABINGWA:ALICHOKISEMA GARETH BALE BAADA YA CRISTIANO RONALDO KUVUNJA REKODI YA MESSI

 Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 30,2014 SAA 04:08 ASUBUHI
Gareth Bale amempongeza Cristiano Ronaldo baada ya mshindi huyo wa Ballon d'Or kuonyesha mchezo wa hali ya
juu kwa Real Madrid katika mchezo wa  ligi ya mabingwa barani ulaya hapo jana.

Real walikamilisha ushindi katika Ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya Bayern Munich kwa kufunga mabao 4-0 katika uwanja wa  Allianz Arena hapo jana kwa kukamilisha jumla ya mabao 5-0 na kujipatia nafasi ya kucheza fainali mwezi ujao mjini Lisbon.

Sergio Ramos aliingia nyavuni mara mbili mfululizo kwa haraka kwa kufunga katika dakika ya  dakika 16 na 20 kabla ya Ronaldo kufunga ya kwake mawili pia katika dakika ya 34 na 90.

Nyota wa kimataifa kutoka Ureno Cristiano Ronaldo alivunja rekodi ya Lionel Messi ya ufungaji mabao mengi zaidi kwa kufunga bao lake la 15 na 16 msimu huu, katika mechi kumi za ligi hiyo ya mabingwa Barani Ulaya mara mbili zaidi ya Lionel Messi wa Barcelona .

Bale aliiambia Sky Sports News: "Hivyo ni kwa nini yeye ni mchezaji bora duniani, Ni heshima kwa kucheza pamoja naye na kujifunza kutoka kwake".
"Tumekuwa bado tukicheza mechi kwa pamoja na tumaini anaweza kufunga mara nyingi zaidi."
Real sasa watakutana na aidha wapinzani wao wa mji Atletico au Chelsea ya bosi wao wa zamani Jose Mourinho katika fainali, lakini Bale anajua kuwa watakabiliana na changamoto katika mchezo unaokuja.
Aliongeza: "Ni timu  mbili zote kubwa, sidhani kama tunaweza kuchagua Mtu wa kucheza naye, mimi nina uhakika itakuwa final kubwa".
"Wote tutaweza kuzingatia mchezo na matumaini yetu ni  kufanya vizuri siku hiyo" alisema Gareth Bale.

Post a Comment

0 Comments